1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Baraza la Wawakilishi Marekani lashindwa kuchagua spika

4 Januari 2023

Kiongozi wa chama cha Republican nchini Marekani, Kevin McCarthy, ameshindwa kupata kura za kutosha ili kuchaguliwa kuwa spika wa Baraza la Wawakilishi baada ya duru tatu za upigaji kura

USA US-Repräsentantenhaus Wahlen
Kevin McCarthy Picha: KEN CEDENO/UPI Photo/IMAGO

Katika duru ya kwanza, wajumbe 19 waliasi kutoka chama chake na katika duru mbili zilizofuatia, McCarthy alishindwa kupata kura za kutosha kutoka kwa Warepublican wenzake.

McCarthy amewaambia waandishi wa habari kuwa rais wa zamani, Donald Trump, alimpigia simu na kusisitiza kumuunga mkono, lakini kilichoshuhudiwa bungeni sicho alichokitarajia.

"Kuna mambo mengi tulitaka kufanya. Tulitaka kuweka idadi ya kesi za uchunguzi tulizonazo. Tulitaka kuona vikao mbalimbali vya kamati tulizonazo. Hakuna kati ya hayo kilichotendeka. Lakini kama tutaweza kutatua tofauti zetu, na mara hii tufaulu, tutakuwa na nguvu zaidi na kukamilisha mambo tunayotaka kuyafanya," amesema McCathy

Mwanasiasa huyo kutoka California alihitaji kura 218 kati ya 434. Hii ni mara ya kwanza katika karne moja, kwa Warepublican kushindwa kumchagua spika hata baada ya majaribio matatu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW