1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Barca wakwea hadi nafasi ya pili La Liga

8 Februari 2021

Hatua ya kocha wa Barcelona Ronald Koeman kuwapumzisha wachezaji wake nyota akiwemo Lionel Messi ililipa baada ya kuwalaza Real Betis magoli 3-2 katika mpambano wa Ligi Kuu ya Uhispania La Liga.

Ronald Koeman
Picha: picture-alliance/DPPI Media/S. Gontha

Koeman amesema alikuwa anawataka wachezaji wake wapumzike kuelekea mechi yao ya nusu fainali ya kombe la Copa del Rey dhidi ya Sevilla.

Lionel Messi lakini aliingia katika kipindi cha pili na kuhakikisha kwamba timu yake inaondoka na pointi tatu. Kwa sasa barca iko nyuma ya vinra Atletico Madrid kwenye msimamo wa La Liga na ndio maana Koeman akaonelea bora aweke umuhimu katika taji la Copa del Rey.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW