Barcelona kumkosa Yamal dhidi ya Newcastle
17 Septemba 2025
Matangazo
Barcelona imesema kuwa Yamal hayumo katika kikosi kinachoelekea England kupambana na Newcastle katika mechi hiyo ya kwanza ya makundi.
Yamal tayari alikuwa ameikosa mechi ya La Liga ya Barcelona mwishoni mwa wiki walipopambana na Valencia na kushinda 6-0, kufuatia jeraha alilopata katika eneo la sehemu nyeti.
Kocha wa Barca Hansi Flick amesema alighadhabishwa na hatua ya timu ya taifa ya Uhispania kumchezesha Yamal katika mechi zao za kuwania kufuzu Kombe la Dunia ambazo walizishinda kwa urahisi.
Nyota huyo alipata jeraha hilo wakati wa mechi hizo za kimataifa.