1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Barcelona watetereka, Madrid wakwea kileleni

27 Novemba 2023

Barcelona walilazimishwa sare ya 1-1 na Rayo Vallecano mjini Madrid katika La Liga na kutoa nafasi kwa Real Madrid kuparamia kileleni mwa ligi hiyo.

Uhispania Jude Bellingham
Kiungo wa Real Madrid Jude Bellingham akisherehekea kufunga goliPicha: Josep Lago/AFP/Getty Images

Hii ni kufuatia ushindi wa Madrid wa 3-0 dhidi ya Cadiz ambapoJude Bellingham alifunga goli kwa mara nyengine tena na Rodrygo akapachika kimyani mawili.

Atletico Madrid walimuhitaji kwa mara nyengine mshambuliaji wao mahiri Antoine Griezmann ili kupata pointi tatu muhimu walipokuwa wakichuana na Real Mallorca.

Griezmann kunako dakika ya 64 ya mechi alifunga goli la pekee hilo likiwa lake la tisa msimu huuna kuhakikisha kwamba, wanaruka hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo.

Griezmann yuko bao moja tu nyuma ya kiungo wa Madrid Jude Bellingham.

Vyanzo: AP/Reuters

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW