1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SayansiUkraine

Baridi kali na barafu yasababisha umeme kukatika Ukraine

9 Januari 2024

Wasimamizi wa gridi ya kusambaza umeme nchini Ukraine wamesema hali mbaya ya hewa ya baridi kali imesababisha zaidi ya miji na vijiji 1000 kukosa umeme katika mikoa tisa ya nchi hiyo.

Hali mbaya ya hewa ya baridi kali na barafu yasababisha umeme kukatika katika miji chungunzima Ukraine
Hali mbaya ya hewa ya baridi kali na barafu yasababisha umeme kukatika katika miji chungunzima UkrainePicha: Oleh Tymoshenko/ZUMA Wire/IMAGO

Shirika la umeme Ukrenegro limewatolea mwito wananchi kutumia vizuri umeme kipindi hiki ambapo mfumo wa usambazaji umeme umedhoofishwa na mashambulizi ya Urusi.

Shirika hilo limetanabahisha kwamba matumizi ya umeme yalikuwa yamefikiwa viwango vya juu kabisa wiki hii kutokana na kushuka kwa viwango vya joto katika maeneo mengi ya nchi hiyo.

Hali ya baridi na upepo mkali pamoja na barafu imesababisha kukatwa kwa nguvu za umeme katika makaazi 1,025.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW