Bashir aahidi kuliunga mkono taifa jipya la Sudan Kusini
29 Desemba 2010Rais wa Sudan Omar Hassan al-Bashir ameahidi kulisaidia eneo la Kusini kuwa taifa lililostawi na imara endapo kura ya maoni ya mwezi ujao itaamua ijitenge na kujisimamia yenyewe.Katika hotuba maalum ya televisheni aliyoitoa akiwa eneo la Gezira, Rais Bashir alisema atakuwa wa kwanza kuitambua nchi hiyo endapo matokeo yataashiria kujitenga.
Kauli hizo zimepokelewa vizuri na katibu mkuu wa kundi la waasi wa zamani SPLM,Pagan Amum.Wakazi wa Eneo la Kusini mwa Sudan wanajiandaa kupiga kura ya maoni mnamo tarehe 9 itakayoiamua hatma yake itakayoitimiza azma yake ya kutaka kujitenga.
Kiasi ya wapiga kura milioni 3.5 wamesajiliwa kushiriki katika kura hiyo ya maoni.Wakati huohuo katibu mkuu wa Umoja wa Nchi za Kiarabu Amyr Moussa anaikamilisha ziara yake ya siku mbili nchini Sudan alikokutana na viongozi wa kuisni na kaskazini.