1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayer Leverkusen yabeba Kombe la Super Cup la Ujerumani

18 Agosti 2024

Mabingwa wa ligi ya Ujerumani, Bayer Leverkusen, wameicharaza Stuttgart 4-3 kwa mikwaju ya penalti katika mechi ya ufunguzi wa msimu wa Super Cup ya Ujerumani jana Jumamosi, na kushinda kombe hilo kwa mara ya kwanza.

Bayer Leverkusen - VfB Stuttgart
Leverkusen, Mabingwa wa DFL Super CupPicha: Bernd Thissen/dpa/picture alliance

Mabingwa wa ligi ya Ujerumani, Bayer Leverkusen, wameicharaza Stuttgart 4-3 kwa mikwaju ya penalti katika mechi ya ufunguzi wa msimu wa Super Cup ya Ujerumani jana Jumamosi, na kushinda kombe hilo kwa mara ya kwanza.

Kwenye dakika ya 11 ya mchezo, Leverkusen, kupitia kwa Victor Boniface, waliandikisha goli la kwanza kabla ya Millot wa Stuttgart kusawazisha dakika nne baadaye.

Soma zaidi. Andrich asaini mkataba mpya wa kusalia Leverkusen hadi 2028

Katika dakika ya 63, Stuttgart walipata goli la pili kabla ya Leverkusen kusawazisha katika dakika ya 88 na kupelekea mchezo huo kwenda kwenye matuta ambayo yaliwapa ushindi Leverkusen na kuweka rekodi ya kutofungwa mchezo wowote kwenye uwanja wao wa nyumbani tangu mwezi Mei mwaka uliopita.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW