1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayern, Dortmund zaendeleza ushindi

Admin.WagnerD23 Februari 2016

Bayern Munich iliweza kupata ushindi wa kuridhisha wa mabao 3-1 dhidi ya timu iliyopanda daraja msimu huu ya Darmstadt na kulinda uongozi wake wa pointi nane kileleni mwa ligi

Bundesliga Bayern München gegen SV Darmstadt 98 Thomas Müller Fallrückzieher
Picha: imago/J. Huebner

Thomas Muller alikuwa shujaa wa Bayern siku ya Jumamosi kwa kufunga mabao 2. "Kama hufungi magoli, hilo ni tatizo kubwa. Iwapo kwa wapinzani wetu tunafungwa bao katika hali kama walivyofanya Darmstadt , kwa kweli ni tatizo. Lakini tulikuwa tunajiamini. Pamoja na hayo ilibidi kubadili hali ya mchezo huo. Timu inastahili sifa, lakini kutokana na kupoteza nafasi nyingi za kufunga , tulitarajia hali nyingine kabisa".

Borussia Dortmund imejiimarisha katika nafasi ya pili, ikifungua mwanya wa pointi 15 kutoka timu iliyoko katika nafasi ya tatu Hertha Berlin kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Bayer Leverkusen , timu ambayo iko katika nafasi ya nne.

Mchuano kati ya Leverkusen na Dortmund ulikuwa wa hisia nyingiPicha: picture-alliance/dpa/M. Becker

Mchezo huo ulisimama kwa muda baada ya kocha wa Leverkusen Roger Schimidt kukataa kutoka uwanjani na kukaa kwa mashabiki kufuatia kuondolewa na refa baada ya kubishana na refa Felix Zwayer. Kocha Roger Schimdt anakabiliwa na adhabu kutoka shirikisho la soka la Ujerumani, ambalo linaanza kikao chake cha uchunguzi kuhusu tukio hilo leo Jumatatu.

Hata hivyo baada ya dakika tisa mchezo huo kusimama, mwamuzi aliendelea na mchezo huo na hadi mwisho Dortmund iliibuka na ushindi wa bao 1-0.

TSG Hoffenheim ambayo ilikuwa ikishikilia mkia katika msimamo wa ligi ya Ujerumani imejitutumua na kusogea hadi nafasi ya 17 kutoka mkiani ikiiacha Hannover 96 ikishikilia mkia.

Hoffenheim ambayo imetupa maumaini yake kwa kocha kijana kabisa katika bundesliga Julian Nagelsmann mwenye umri wa miaka 28, ambaye katika mchezo wake wa pili ameweza kunyakua pointi nne baada ya timu yake kupata ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Mainz 05 siku ya Jumamosi. "Hali ilikuwa ya msisimko mkubwa mwishoni baada ya ushindi wa mabao 3-2. Nafikiri , nadhani niliangalia mara 7000 saa yangu ya mkononi , wakati wa dakika 3 za mwisho zilipokwisha. Saa ilikuwa haiendi kwa haraka. Na sikuwa naona vizuri mishale ya saa yangu. Na mwishoni tulikuwa na furaha, wakati firimbi ya mwisho ilipowadia.

Mwandishi: Sekione Kitojo / dpae / afpe / rtre
Mhariri: Yusuf , Saumu