1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayern kuanza msimu dhidi ya Frankfurt

Josephat Charo
17 Juni 2022

Mabingwa wa Bundesliga Bayern Munich watakuwa na kibarua kipevu ugenini Frankfurt katika mechi ya kwanza ya msimu wa 60 wa Bundesliga Ijumaa Agosti 5.

Bundesliga | FC Bayern München v VfB Stuttgart
Picha: Michael Probst/AP/picture alliance

Bayern Munich itaanza kampeni ya kutafuta taji la 11 mfululizo la Bundesliga na mechi ngumu ugenini dhidi ya mabingwa wa ligi ya Ulaya, Eintracht Frankfurt. Frankfurt imeshinda mechi mbili kati ya tatu walizocheza na Bayern kabla mechi hiyo itakayochezwa Ijumaa Agosti 5, ambayo itafungua pazia la msimu wa maadhimisho ya miaka 60 ya Bundesliga.

Ratiba ya msimu mpya wa 2022-23 imetolewa Ijumaa. Timu iliyokamilisha msimu uliopita katika nafasi ya pili, Borussia Dortmund, itaanza kampeni yake dhidi ya Bayer Leverkusen Agosti 6 au 7. Kwa timu zilizopanda daraja, Schalke itaanza ugenini Cologne na Werder Bremen inatarajiwa kuanza ugenini dhidi ya Wolfsburg.

Kutakuwa na zaidi ya miezi miwili bila mechi katikati ya msimu wa 60 wa Bundesliga kwa sababu ya kombe la dunia nchini Qatar. Bundesliga itaanza kipindi cha mapumziko ya msimu wa baridi mapema kuliko ilivyo kawaida mnamo Novemba 13 na itarejea viwanjani Januari 20 mwakani.

(ap)

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW