1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayern kumnasa Kane hatimaye?

31 Julai 2023

Vyombo vya habari Ujerumani vinaripoti kuwa Afisa Mkuu Mtendaji wa Bayern Munich Jan-Christian Dreesen na mkurugenzi wa kiufundi wa klabu hiyo Marco Neppe, wanasafiri London Jumatatu ili kusukuma usajili wa Harry Kane.

FC Bayern München erklärt England-Star zum Transfer-Ziel-Nummer 1.
Picha: Sven Simon/picture alliance

Inaripotiwa pia kwamba wakuu hao wa Bayern pia watawasilisha ombi jengine la zaidi ya pauni milioni 80 baada ya ombi lao la kwanza kukataliwa na mkuu wa Spurs Daniel Levy.

Levy alikuwa hataki kumuachilia Kane ila mmilki wa klabu hiyo ya London Kaskazini Joe Lewis anadaiwa kumwambia Levy amuuze Kane mwenye umri wa miaka 30 iwapo hataki kuongeza kandarasi.

Vyanzo: Reuters/DPAE/AP

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW