1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayern Munich kuchuana na PSG robo fainali Champions League

19 Machi 2021

Mabingwa watetezi wa michuano ya klabu bingwa barani Ulaya Bayern Munich watachuana na Paris St-Germain katika mchezo wa robo fainali ya Champions League msimu huu.

Champions League Auslosung
Picha: UEFA/REUTERS

Borussia Dortmund itakuwa na kibarua dhidi ya Manchester City ya Uingereza.

Chelsea inayotiwa makali na Thomas Tuchel, itachuana na klabu ya Ureno ya Porto alafu Real Madrid ya Uhispania itazipiga na Liverpool ya Uingereza.

Mechi kati ya Bayern Munich na Paris St-Germain ni marudio ya fainali ya Champions League msimu uliopita wakati Bayern ilipoifunga PSG bao 1-0, bao lililofungwa na mchezaji wa zamani wa PSG Kingsley Coman.

Fainali ya mwaka huu itachezwa mnamo Mei, 29 katika uwanja wa Atatürk Olympic mjini Istanbul, Uturuki.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW