1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayern Munich na Bochum

3 Oktoba 2008

Mpambano kati ya Munich na Bochum katika Bundesliga utaiokoa Munich ?

B.Munich ilipolazwa na Hannover.Picha: AP

Maadui zao Bochum,wakipesuka mkiani mwa Ligi kwahivyo, waweza wakageuka leo mhanga mbele ya Munich . Kileleni mwa Ligi kumesheheni. Pointi 3 tu zikitenganisha timu 7 za usoni kabisa:

Hamburg wanaongoza Ligi, hawakutamba sawa sawa walipoondoka na ushindi wa bao 1:0 nyumbani wiki iliopita,lakini kocha wao Martin Jol, ataridhika ikiwa kesho Hamburg, itashinda tena kwa bao hilo hilo 1 huko Cottbus.Schalke inasimama nafasi ya 4 na inakutana na Wolfsburg .Borussia Dortmund iliopo nafasi ya 5 iko nyumbani ikiikaribisha kesho Hannover.Bayer Leverkusen ikinyatia kutoka nafasi ya pili huenda ikaubakua usukani wa Ligi alao kwa masaa 24 ikiitimua Hertha Berlin.Werder Bremen ikiwa nafasi ya tatu ya ngazi ya Ligi ina kibarua kigumu huko Stuttgart wakati Hoffenheim inapanga kuitoa jasho Frankfurt.

Kwa mashabiki wa Mto Rhine, mahasimu 2 wa mtaani FC Cologne na Borussia Moenchengladbach wanakumbana na timu hizi mbili za asilia zinapokutana ziumiazo ni nyasi.Kocha wa Borussia, Luhakay anahitaji ushindi ili kuepuka shoka.Kwani, baada ya kushindwa mechi 3 mfululizo, ushindi dhidi ya Cologne ilioilaza Schalke mwishoni mwa wiki iliopita na kuitungua kileleni,hautakua rahisi.

Katika Premier League-Ligi ya Uingereza timu 3 za kileleni-Chelsea,Liverpool na Aston villa ,zitakuwa uwanjani kesho jumapili,Arsenal ndio inayokodolewa macho leo:Mahasimu wao ni Sunderland n a lazima watambe kwani pigo jengine kama lile la mwishoni mwa wiki iliopita kutoka chipukizi Hull city,litazika matumaini ya Arsenal ya kuzikamata Chelsea na Liverpool kileleni.

Chelsea ina kibarua kigumu kesho itapokumbana na Aston villa iliopo nafasi ya 3.Wachezaji wake kadhaa wameumia au hawawezi kucheza.Kuanzia stadi wa Ivory Coast Didier Drogba hadi mghana Michael Essien; na hata Deco,Carvalho na Joe Cole pia hawamo.Liverpool kama Chelsea bado haikushindwa msimu huu na wanatarajia pointi 3 kutoka Manchester City inaoendelea kuonesha ukarimu wa pointi.

Mabingwa Manchester United, wangali wamenasa kati kati ya Ligi wakitumai pointi 3 kutoka Blackburn Rovers zitaanza kuwasukuma kileleni.Kwa bahati mbaya lakini,Paul Scholes ameumia na hatima ya Wayne Rooney haijulikani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW