1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayern munich sare na Hamburg 1:1

25 Februari 2008

Wakati Bayern Munich imemudu suluhu bao 1:1 na Hamburg katika Bundesliga,Hotspurs imeivua taji la FA chelsea (2:1)

Hamburg na B.MunichPicha: AP

Bayern Munich nusra jana ikione cha mtema kuni ilipomudu suluhu tu nyumbani ya bao 1:1 na Hamburg.

Tottenham hotspurs imeitia munda Chelsea na kutotoka jana na kombe la ligi la FA wakati Manchester United imepunguza mwanya na Arsenal kileleni hadi pointi 3.

Tukianza na Ligi mashuhuri za ulaya, Bayern Munich walitazamiwa jana kupanua mwanya wao kileleni hadi pointi 6 kati yao na Bremen baada ya Bremen kuteleza jumamosi kwa kuzabwa bao 1:0 na Frankfurt.

Munich ambayo kati ya wiki hii ina miadi na mahasimu wao wa mtaani-Munich 1860 katika kombe la shirikisho la dimba la Ujerumani, haitamudu kupoteza pointi 3 nyengine jumamosi ijayo itapoitembelea Schalke 04 inayosimama nafasi ya 5 ya ngazi ya ligi.

Makocha wa timu hizo mbili Ottmar Hitzfeld na Huub Stevens hawakuridhika na sare hiyo ,kwani kila mmoja akihisi timu yake ilistahiki jana kushinda.Hitzfeld:

„Haikutosha kuondoka na ushindi,lakini ikiwa wataka kushinda mpambano mkali kama ule ,basi yakupasa kueouka makosa kama tuliofanya .kwa hali hiyo,inatubi kuridhika na sare ya bao 1:1.“

Nae kocha wa Hamburg Huub Stevens alielezea kutoridhika kwake hivi:

„Ilibainika wazi mpira ulikuwa wetu kurusha.Hatahivyo ilitupasa kuwa macho na kutoonesha uzembe kama tulioonesha tukilalamika tu badala ya kuendelea kucheza na hivyo tukawapa nafasi B.Munich kusawazisha.”

Katika Premier League –Ligi ya Uingereza,Manchester united imepunguza mwanya kati yake na Arsenal hadi pointi 3 .Manchester iliirarua Newcastle kwa mabao 5-1 .Birmingham iliizima Arsenal na vishindo vyake hadi kutoka sare 2-2.Kocha wa Manchester united Sir Alex Ferguson aliipongeza MANU kwa jinsi ilivyotamba baada ya kufuta madhamgbi ya jumamosi iliopita ilipolazwa na Manchester City.

Chelsea ilikua uwanjani Wembley kutaka kuvaa taji lao la kwanza msimu huu na kutetea ubingwa wao wa kombe la Ligi la FA .Lakini, waliula na chua kwa uvivu wa kuchagua.Baada ya Didier Drogba kulifumania lango la Tottenham Hotspurs kwa bao la free-kick, Hotspurs waliwaambia kutangulia si kufika.Baada ya kusawazisha kwa mkwaju wa penalty na kurefusha mchezo, walijipatia bao la pili na la ushindi na kuitoa nje Chelsea mikono mitupu.Kweli mpira unadunda.

Katika Serie A,Ligi ya italic uongozi wa Inter Milan kileleni ulipunguzwa jana hadi pointi 9 baada ya mabingwa hao wa Itali kutoka sare tu bao 1-1 na sampdoria.Roma, inayofuata nafasi ya pili iliondoka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Fiorentina.

Katika la Liga-ligi ya Spain ,kocha wa Real Madrid -mjerumani Bernd Schüster,kocha wa zamani wa Getafe msimu uliopita, alibidi kuadhibiwa kwa kuidharau Getafe. Getafe iliikomea Real bao 1:0 na kuwavunjia rekodi yao ya kutoshindwa nyumbani katika changamoto za La Liga.

Kocha wa FC Barcelona Frank Rijkaard hakuweza kuficha furaha yake kwa kuiona timu yake ya FC Barcelona ikiichapa Levante mabao 5-1.Simba wa nyika-mkameroun Samuel Eto’o alitia pekee mabao 3-hattrick.

Mabondia:

Muukraine mwenye kambi yake nchini Ujerumani, Wladmir Klitschko-bingwa wa taji la dunia la wezani wa juu ulimwenguni la IBF alimtandika makonde bingwa wa dunia wa wezani wa juu wa taji la WBO-world Boxing Organisation mrusi Sultan Ibragimov na kumpkonya taji kwa pointi.

Madume hao 2 walitimuana kwa duru 12 kabla Klitschko kutangazwa mshindi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW