1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayern Munich yajiimarisha ligi ya mabingwa Ulaya

7 Novemba 2024

Klabu ya Bayern Munich imeendelea kujiimarisha katika azma yake ya kutaka kufuzu michuano ya kombe la mabingwa Ulaya, Champions, baada ya hapo kupata ushindi mwembamba wa bao moja kwa bila dhidi ya Benfica Lisabon.

Wachezaji wa Bayern wakisherehekea goli
Wachezaji wa Bayern wakisherehekea goliPicha: Foto Huebner/picture alliance

Klabu ya Bayern Munich imeendelea kujiimarisha katika azma yake ya kutaka kufuzu kwa duru ya mtoano katika michuano ya kombe la mabingwa Ulaya, Champions, baada ya hapo jana kupata ushindi mwembamba wa bao moja kwa bila dhidi ya Benfica Lisabon.

Timu nyingine ya Ujerumani, Stuttgart, ilikula kichapo cha goli mbili kwa bila nyumbani dhidi ya Atalanta.

Barcelona ya Uhispania yenyewe ilitoka kifua mbele baada ya kuibuka na ushindi mnono wa mabao 5-2 dhidi ya Red Star Belgrade.

Na huko Paris, timu ya PSG iliendelea kujikongoja kwenye mbio hizi za ubingwa baada ya kufungw amabao 2-1 na Atletico Madrid wakiwa nyumbani na kuwaacha vinara hao wa Ligue 1 kuwa hatarini kuenguliwa kwenye michuano hiyo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW