Bayern Munich yajiimarisha kileleni mwa ligi ya Bundesliga
17 Februari 2020Bayern Munich ikifukuzia ubingwa wake wa nane mfululizo katika Bundesliga , inafuatiwa na RB Leipzig ambayo ilikandika Werder Bremen mabao 3-0 siku ya Jumamosi na kuendelea na mbio za kuifukuza Bayern Munich kileleni.Mlinda mlango wa Bayern Manuel Neuer amesema wangeweza kupachika hata mabao 10 lakini hata sisi tungefungwa mabao kiasi. Mshambuliaji wa Bayern Munich Thomas Mueller alikuwa na haya ya kusema.
"Tulianza vizuri sana, tulifurahia kiuchezaji. Mwanzoni tulifanya kazi nzuri sana, na kabla ya mapunziko kiukweli tungeweza kuwa na mabao matano, au sita kwa sifuri. Ndio sababu kimsingi tumefurahi sana, na kazi yetu uwanjani tumeitimiza kikamilifu, tumerejea tena kuwa vinara wa ligi. Ugenini hapa Koln , bila shaka tumekuwa timu iliyotamalaki, lakini kila mara ugenini ni lazima kupata pointi tatu. Kipindi cha pili bahati mbaya ni kama baadhi ya vipindi vya pili huko nyuma. Tulikuwa mbali na hali tuliyokuwa nayo , baada ya kuongoza kwa mabao 4-0 tulitakiwa kuweka mbinyo zaidi.Na hili katika michezo iliyopita kila mara tulishindwa kuendelea na mchezo wetu hadi mwisho."
Kocha wa FC Koln Markus Gisdol amesema katika kipindi cha kwanza unaweza kuona kuwa bado tumo katika awamu ya kujijenga." Bayern ilitumia uwezo wake vizuri sana, Tulikuwa wenye kusita sita sana, tuliwapa eneo kubwa la kufanya watakavyo na hatukwenda mbele kwa kujiamini vya kutosha. Huyu hapa Markus Gisdol.
"Ndio nafikiri ilikuwa kipindi chote cha kwanza, ambapo tulikuwa na matatizo makubwa, kuweza kuwadhibiti. Bayern walikuwa katika kiwango cha juu kabisa kuanzia mwanzo. Katika kipindi cha kwanza hatukuweza kupata njia muafaka, na tulitoa nafasi kubwa , na hatukufanya vizuri katika kila nafasi. Na ndio Bayern ikiwa katika kiwango cha juu kwa sasa waliweza kutimiza kila wanalotaka, na hii ilitokea kwa haraka sana."
Werder Bremen ambayo iliiondoa Borussia Dortmund katika kinyang'anyiro cha kombe la shirikisho DFB Pokal, na kucheza kandanda safi , haifanyi vizuri hata hivyo katika ligi ya Bundesliga. Ikiwa katika nafasi ya 17 na pointi 17 tu imo katika hatari ya kurejea katika daraja la pili msimu ujao. Jumamosi ilikumbana na timu iliyoko katika nafasi ya pili ya Bundesliga RB Leipzig na ulikuwa mtihani mkubwa kwa kocha Florian Kohfeldt kuweza kubadilisha majaaliwa ya timu hiyo. Lakini ikiwa ugenini Werder Bremen ilipokea kipigo cha mabao 3-0. Kocha wa RB Leipzig Julian Nagelsman anasema.