1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayern Munich yatawazwa mabingwa Champions League

24 Agosti 2020

Bayern Munich imenyakua ubingwa wa Champions League kwa mara ya sita baada ya kuifunga PSG bao moja kwa nunge katika fainali iliyochezwa usiku wa kuamkia leo mjini Lisbon, Ureno.

Champions League Finale 2020 Paris vs Bayern München | Sieger Bayern München
Timu ya Bayern Munich ikishangilia ushindi wa Champions League Picha: Getty Images/AFP/M. Childs

Bao la ushindi lilipachikwa wavuni katika dakika ya 59 na mshambuliaji Kingsley Coman aliyewastaajabisha mahasimu wao klabu ya PSG ya Ufaransa iliyokuwa ikimezea taji hilo la klabu bingwa barani Ulaya.

Bayern ambayo ilinyakua pia ubingwa wa ligi ya kandanda ya Ujerumani Bundesliga, imeondoka na kikombe cha Champions League kwa fahari baada ya kutopoteza mchezo hata moja kwenye mashindano hayo.

Mamia ya wafuasi wa klabu hiyo katika mji wa nyumbani wa Munich walisherehekea ushindi wa timu yao kwa kumiminika barabarani wakipuliza firimbi na honi za magari.

Wakati huo huo polisi mjini Paris ililazimika kutumia mabomu ya machozi na nguvu za wastani kuwatawanya mamia ya mashabiki wa klabu ya PSG waliozusha vurugu baada ya timu hiyo kupoteza mchezo na Bayern na kulikosa kombe la Champions League.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW