1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayern wapepea, Dortmund vichwa chini nyumbani kwao

30 Novemba 2020

Ligi Kuu ya Ujerumani Bundesliga ilishuhudia RB Leipzig kuwawekea shinikizo Bayern Munich baada ya kuwalaza Arminia Bielefeld 2-1 Borussia Mönchengladbach wakivuna ushindi mkubwa wa 4-1 walipokuwa wenyeji wa Schalke 04.

Bundesliga I Borussia Dortmund v Bayern München
Picha: Leon Kuegeler/Pool/REUTERS

Bayern Munich walikuwa ugenini wakikwaana na VfB Stuttgart na walipata ushindi wa tatu moja. Leon Goretzka ni kiungo wa Bayern na alikuwa na haya ya kusema baada ya mpambano huo.

"Kwa sasa tunafanya makosa mengi tu tuwapo na mpira. Ila nafikiri tulipata motisha kwa mara nyengine tena na tukatumia nafasi zetu vyema. Na kwa Douglas Costa tuna mchezaji mwenye uwezo mkubwa tunayeweza kumleta na kwa nafasi moja tu aliyopata tukapata goli la tatu."

Borussia Dortmund walikuwa katika uga wao wa nyumbani Signal Iduna Park wakiwakaribisha FC Köln na hao BVB walishangazwa kwani walicharazwa mbili moja, huku Erling Haaland mshambuliaji nyota wa Dortmund akikosa kutamba katika mpambano huo.

Huyu hapa kocha wa Dortmund Lucien Favre.

"Bila shaka sote tumevunjwa moyo kwa kupoteza leo dhidi ya Köln nyumbani. Bila shaka ni vigumu kukubali hilo."

Kocha wa Dortmund Lucien Favre (kushoto)Picha: Annegret Hilse/REUTERS

Na mechi nyengine ya Bundesliga iliyokuwa na msisimko mkubwa ilikuwa kati ya Union Berlin na Eintracht Frankfurt. Mchuano huo ulishuhudia jumla ya magoli sita baada ya timu hizo kutoka sare ya magoli matatu.

Max Kruse ni mshambuliaji wa Union Berlin na alifunga goli la kusawazisha katika mechi hiyo na kuwavunja moyo Frankfurt.

"Kwasababu tulikuwa chini 2-3 katika dakika kumi na tano zilizopita, nafikiri ni alama muhimu tuliyoipata. Ila ukiuangalia mchezo mzima nafikiri katika dakika ishirini za kwanza tulikuwa tumeudhibiti mchezo vyema na tungeweza kupata ushindi wa mapema. Tulijikita sana katika kujilinda ila hilo halikutufaa sana lakini katika kipindi cha pili tulicheza vyema pia na tukasawazisha ikawa magoli matatu kwa matatu. Na kwasababu hiyo nafikiri tunastahili kuipata pointi hii."

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW