1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayern watamba, Leipzig wasakamwa

18 Mei 2020

RB Leipzig walitoka sare ya goli moja na SC Freiburg nyumbani kwao Red Bull Arena na Hoffenheim licha ya kuwa nyumbani walilelemewa tatu bila na Hertha Berlin nao Fortuna Düsseldorf na Paderborn wakatoka sare bila bila.

Deutschland Bundesliga RB Leipzig gegen Freiburg
Picha: Reuters/J. Woitas

Wolfsburg walikuwa ugenini wakicheza na Augsburg na wakatoka huko na ushindi wa mbili moja na mpambano wa mwisho Jumamosi uliwapatanisha Eintracht Frankfurt na Borussia Moenchengladbach na Gladbach wakaebuka kidedea tatu moja.

Hapo Jumapili mabingwa watetezi ambao pia ni vinara waliingia uwanjani kuchuana na Union Berlin na waliebuka washindi wa mbili bila Robert Lewandowski na Benjamin Pavard wakifunga mabao hayo ya Bayern na FC Cologne walipoteza nafasi za wazi katika mechi yao na Mainz iliyoishia sare ya magoli mawili.

Robert Lewandowski baada ya kufunga mkwaju wa penaltiPicha: Reuters/H. Hanschke

Kwa sasa Bayern Munich ndio wanaoongoza ligi wakiwa na pointi hamsini na nane baada ya mechi ishirini na sita kisha watani wao Borussia Dortmund wanawafuata kwa pointi hamsini na nne. Borussia Moenchengladbach wao ni wa tatu wakiwa na alama hamsini na mbili na Leipzig wanawafuata wakiwa alama moja nyuma. Chini ya jedwali kuna Dusseldorf katika nafasi ya kumi na sita wakifuatwa na Werder Bremen na wanaovuta mkia ni Paderborn.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW