1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayern yaikaanga Schalke 8 - 0 katika ufunguzi wa msimu

19 Septemba 2020

Msimu mpya wa ligi kuu ya kandanda Ujerumani - Bundesliga ulianza katika uwanja mtupu jana usiku huku bingwa mtetezi Bayern Munich akimnyesha Schalke mvua ya magoli 8 - 0 katika mechi ya ufunguzi.

Fussball Bundesliga - Bayern Munich vs. Schalke 04
Picha: Michael Dalder/Reuters

Winga wa Ujerumani Leroy Sane alikuwa nyota wa mchezo na akafunga bao katika mechi yake ya kwanza ndani ya uzi wa Bayern na Jamal Jamal Musiala akwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi wa Bayern kuwahi kufunga bao akiwa na umri wa miaka 17

Serge Gnabry alifunga hat trick na Sane akatoa asisti mbili kati ya mabao hayo. Mabao mengine yalifungwa na Leon Goretzka, Thomas Muller na Robert Lewandowski

Schalke haijashinda katika mechi 17 mfululizo wakati Bayern ikiendeleza rekodi yake ya kushinda mechi 22 mfulululizo. Mipango ya Bayern kuwaruhusu mashabiki 7,500 kuhudhuria mechi hiyo dimbani ilifutwa na mamlaka za afya mjini Munich kutokana na kuongezeka kwa maambukizi ya corona.

Hii leo, Borussia Dortmund watakuwa na mashabiki 10,000 katika uwanja wao wa Signal Iduna Park wakati wakiwakaribisha Borussia Moenchengladbach, wakati FC Cologne wakiwaruhusu mashabiki 6,200 katika mechi yao dhidi ya Hoffenheim. DW Kiswahili itakuletea matangazo ya moja kwa moja ya mechi kati ya Werder Bremen na Hertha Berlin

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW