1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayern yatinga robo fainali Kombe la Shirikisho

4 Desemba 2025

Tumalizie michezoni ambapo Bayern Munich waliwazidi nguvu Union Berlin 3-2 mjini Berlin na kufuzu kwenye robo fainali ya mashindano ya kombe la Shirikisho la Ujerumani, DFB Pokal, usiku wa kuamkia Alhamis.

DFB-Pokal 2025 | Achtelfinale | 1. FC Union Berlin vs. FC Bayern München | Eigentor von Diogo Leite
Picha: Odd Andersen/AFP

Kocha wa Bayern Vincent Kompany alianzisha kikosi cha kwanza chenye wachezaji mahiri, akifahamu fika kuwa Berlin ndiyo timu iliyotilia kikomo msururu wao wa kushinda mechi katika Ligi Kuu ya Ujerumani Bundesliga wiki chache zilizopita, walipowalazimisha sare ya mabao mawili.

Lakini katika mechi ya jana, Berlin walijifunga mabao mawili kisha bao la tatu la Bayern likatiwa kimyani na mshambuliaji wao Harry Kane.

Mabingwa wa kombe hilo la shirikisho VfB Stuttgart walipata ushindi wa 2-0 walipokuwa wakipambana na Bochum halafu Freiburg wakailaza Darmstadt 2-0 pia. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW