1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiKimataifa

Bei ya mafuta yapanda kutokana na mzozo Mashariki ya Kati

2 Machi 2026

Bei ya mafuta imepanda leo Jumatatu huku masoko ya hisa yakiropomoka kutokana na kishindo cha mashambulizi ya kijeshi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran yaliyoanza siku ya Jumamosi.

Miundombinu ya usafirishaji mafuta
Mgogoro wa kijeshi unaoshuhudiwa Mashariki ya Kati ndiyo sababu kuu ya kupanda kwa bei ya mafuta. Picha: Bernadett Szabo/REUTERS

Pipa moja la mafuta ghafi limefikia karibu dola 80 kwenye soko la dunia ikiwa ni ongezeko la wastani wa asilimia 7.5 ya bei ya wiki iliyopita.

Wasiwasi ni mkubwa kwamba bei ya nishati hiyo huenda itapanda zaidi mnamo siku zijazo katika wakati hakuna dalili kwa mzozo wa kijeshi wa Mashariki ya Kati kutulia.

Rais Donald Trump wa Marekani ameashiria jana Jumapili kuwa mashambulizi ya nchi yake pamoja na Israel nchini Iran yanaweza kuendelea kwa hadi wiki nne zijazo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW