1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING China itapeleka mjumbe wake kwenda Korea Kazkazini.

17 Februari 2005

China imetangaza kwamba itamtuma mjumbe wake maalumu mwishoni mwa juma kwenda Korea Kazkazini, ambayo juma lililopita ilitangaza ina miliki silaha za kinuklia. Wizara ya mambo ya kigeni imemtaja, Wang Jiarui, kiongozi wa kitengo kinachohusika na ushirikiano wa kimataifa cha chama cha kikomunisti. China inataka Korea Kazkazini ikubali kushiriki katika mazungumzo ya mataifa sita kuhusu silaha za kinuklia. Wapatanishi wa Korea Kusini na Marekani wamekwenda mjini Beijing kushauriana na maafisa wa China. China na Japan zimepuuza matamshi ya kiongozi wa shirika la ujasusi la CIA la Marekani, Porter Goss, kuhusu hatari ya makombora ya Korea Kazkazini.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW