1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING-Condoleezza Rice asema Marekani inafikiria njia mpya za kuibana Korea Kaskazini.

21 Machi 2005

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani,Bibi Condoleezza Rice amesema leo kuwa nchi yake na mataifa marafiki katika eneo la Asia,wanafikiria njia mpya za kuibana Korea ya Kaskazini,iwapo nchi hiyo itaendela na kiburi chake cha kuendela na mipango yake ya kukataa kushiriki katika mazungumzo yanayohusu silaha za kinuklia.

Bibi Rice akimaliza ziara yake katika mataifa ya ASIA pia amedokeza kuwa nchi yake italifikisha suala la Korea Kaskazini katika Umoja wa Mataifa iwapo mazungumzo hayo ya silaha za nuklia yatakwama.

Bibi Rice ameongeza kusema kuwa iwapo itashindikana kulimaliza suala la Korea Kaskazini kwa njia hizo wanazokusudia,basi Marekani itawabidi kufikiria njia nyingine ambazo hata hivyo hakuzitaja

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW