Beijing: Maendeleo katika mazungumzo ya
28 Februari 2004Matangazo
BEIJING: Maendeleo wastani yamepatikana katika yale mazungumzo ya mataifa sita yaliyomalizika mji mkuu wa Uchina kuhusu programu ya kinyuklea ya Korea ya Kaskazini. Wawakilishi wa Marekani, Urusi, Japan na Uchina pamoja na nchi mbili za Korea waliwafikiana ifanyike duru nyingine ya mazungumzo. Pia wamekubaliana kuunda kundi la washauri litakalofafanua maswali ya ubishi, alisema Waziri wa Mambo ya Nje wa Uchina Li Zaoxing. Angeliyaita mawafikiano hayo hatua muhimu, japokuwa alisisitiza pia tafauti kubwa zinazoendelea kuweko, alisema. Katika mkutano huo wa Beijing, Korea ya Kaskazini ilisema itayari kuzuiya programu yake ya kinyuklea. Lakini Marekani inadai kuwa nchi hiyo ya kikomunisti ikomeshe kabisa programu hiyo ya kinyuklea.
