Beijing. Mafuriko yasababisha vifo vya watu kadha China na Brazil.
5 Juni 2005Matangazo
Mafuriko ya kila mwaka nchini China yamesababisha vifo vya watu 204, kwa mujibu wa shirika la habari la nchi hiyo Xinhua. Shirika hilo limesema kuwa wakaazi milioni 17 wameathirika na mafuriko hayo katika majimbo 16.
Wafanyakazi wa kutoa msaada wamepelekwa kuimarisha vizuizi vya maji katika mito na mabwawa.
Nchini Brazil siku tatu za mvua kubwa zimesababisha jimbo la kaskazini mashariki la nchi hiyo la Pernambuco kujaa maji.
Maafisa wa serikali wamesema watu 24 wameuwawa na zaidi ya watu 29,000 hawana mahali pa kuishi.