1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beijing. Mafuriko yauwa watu China na Brazil.

5 Juni 2005

Mafuriko ya kila mwaka nchini China yamesababisha vifo vya watu 204, kwa mujibu wa shirika la habari la nchi hiyo Xinhua.

Shirika hilo limesema kuwa wakaazi milioni 17 wameathirika na mafuriko hayo katika majimbo 16.

Wafanyakazi wa uokozi wamepelekwa kuimarisha vizuizi vya maji katika mito na mabwawa.

Wakati huo huo mvua zilizonyesha kwa muda wa siku tatu nchini Brazil zimesababisha jimbo la kaskazini mashariki ya nchi hiyo la Pernambuco kujaa maji. Maafisa wa serikali wamesema kuwa watu 24 wamekufa na zaidi ya 29,000 hawana mahali pa kuishi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW