1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beijing: Matatizo ya Mazingira katika Uchina yamekithiri.

6 Juni 2006

Serekali ya Uchina imekiri kwamba matatizo ya mazingira katika Uchina hayawezi kudhibitika. Uchumi unaokuwa kwa haraka katika nchi hiyo unasababisha uchafuzi mkubwa wa mazingira na idara ya hifadhi ya mazingira katika Uchina inakadiria kwamba inaigharimu nchi hiyo Euro bilioni 200 kwa mwaka. Jana afisa wa cheo cha juu anayeshughulikia mazingira, Zhu Guangyao, amesema uharibifu wa mazingira unaigharimu Uchina asilimia kumi ya gharama za mazao yake ya ndani. Aliongeza kusema kwamba uchafuzi wa mazingira umefikia viwango vya hatari katika maeneo ya mijini na uchafu wa kutoka viwandani umefanya maji katika miji mikubwa mingi kuwa hayafai kwa matumizi.

Mtu mmoja anayeishi Shanghai anasema:

Hewa katika mji mji maisha ni chafu, majiani hali ni ya kutisha. Mtu anavuta hewa yenye harufu ya petroli pamoja na mavumbi. Magari mengi yanachafua hewa, na yananifanya niwe mgonjwa. Inabidi kupunguza magari. Hilo ndilo suluhisho.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW