1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beijing. Mazungumzo na Korea yavunjika.

16 Septemba 2005

Mazungumzo ya nchi sita yenye lengo la kuishawishi Korea ya kaskazini kuachana na mpango wake wa kinuklia yamevunjika.

Baada ya siku ya tatu ya mkutano huo mjini Beijing, Korea ya kaskazini imetoa taarifa ikisema kuwa kutokukubaliana na Marekani kunazuwia maendeleo katika mazungumzo hayo.

Wajumbe katika mazungumzo hayo, ambayo pia yanajumuisha nchi za Korea ya kusini, Russia, Japan na China wamekuwa wakijadili mapendekezo ambayo yatatoa msaada kwa Korea ya kaskazini ili iweze kuachana na mpango wake huo wa kinuklia.

Lakini Korea ya kaskazini inataka mtambo wa maji wa kinuklia ili iweze kuzalisha umeme.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW