1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING. Mazungumzo yafanyika juu ya sheria za uingizaji wa bidhaa za nguo katika Umoja wa Ulaya

26 Agosti 2005

Maafisa wa China na wa Umoja wa Ulaya wameanza mazungumzo mjini Beijing yatakayo lenga mapatano ya kibiashara yaliyo sababisha kuzuiliwa kwa mamilioni ya bidhaa za nguo kutoka China na maafisa wa forodha wa Umoja wa Ulaya.

Mapatano hayo ya kibiashara yaliyo afikiwa mwezi juni yamesabisha mirundiko ya nguo za bei nafuu kuingia katika jumuiya ya Umoja wa Ulaya kutoka China hasa baada ya kuondoshwa kwa viwango vya uingizaji wa bidhaa za nguo ulimwenguni.

Lakini kwa mujibu wa habari za kibiashara China imeshafikisha ukamilifu wa viwango vipya na hivyo basi kujikuta na malimbikizo ya bidhaa zake katika bandari za Ulaya.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW