1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING : Mzozo wa biashara waendelea

5 Juni 2005

Maafisa wa serikali ya China na Marekani wameshindwa kutatuwa mzozo wao wa kibiashara wakati wa mazungumzo yao mjini Beijing hapo jana.

Upande wa China umesema haufurahii hatua ya Marekani kuweka vikomo kwa bidhaa fulani zinazoagizwa na kuingizwa nchini humo.Hadi sasa Marekani imeweka vikomo kwa aina saba ya bidhaa za nguo za China zinazoingizwa nchini humo wakati Umoja wa Ulaya umetaka kuwa na mazunmguzo rasmi na China juu usafirishaji nchi za nje wa nyuzi zake za kitani na fulana.

Usafirishaji nje wa bidhaa za nguo wa China kwa jumla umeongezeka kwa asilimia 29 katika kipindi cha miezi mitatu ya kwanza ya mwaka huu na shinikizo limekuwa likizidi kuongezeka kwa China kuchukuwa hatua zaidi ya kudhibiti hali hiyo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW