1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Beijing yarekodi mvua kubwa katika kipindi cha miaka 140

2 Agosti 2023

Mji Mkuu wa China, Beijing umerekodi mvua kubwa zaidi kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka 140 katika siku chache zilizopita

China Überschwemmungen durch Taifun Doksuri
Picha: TINGSHU WANG/REUTERS

.Idara ya hali ya hewa ya mji mkuu huo imesema imerekodi milimita 744.8 za mvua kati ya Jumamosi na Jumatano leo asubuhi.Mamlaka ya China jana imeeleza kuwa mvua kubwa iliyonyesha karibu na Beijing imeharibu barabara, kuathiri usambazaji wa umeme na kusababisha vifo vya watu 21 na wengine 26 hawajulikani walipo.Maelfu ya watu wamehamishwa na kupewa hifadhi katika shule na majengo mengine ya umma katika viunga vya Beijing na miji mengine ya karibu.Miongoni mwa maeneo yaliyoathirika zaidi na mvua hizo ni Zhuozhou, mji mdogo unaopakana na Beijing upande wa kusini magharibi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW