1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING:CHINA KUTUMA WANAJESHI LIBERIA

28 Novemba 2003
China imetangaza kutuma polisi na wanajeshi nchini Liberia kujiunga na wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka mataifa mengine katika jitihada za kusalimisha silaha za wapiganaji wa Liberia na kuituliza nchi hiyo. Tangazo hilo linafuatia uamuzi wa Liberia kuvunja uhusiano wake na Taiwan na kuanzisha uhusiano na China.Duru za usalama zinasema polisi watano wa China wanajiandaa kuelekea Liberia hapo Jumapili na kwamba kikosi cha China nchini humo hatimae kitafikia wanajeshi 1,200. Hapo mwezi wa Septemba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeidhinisha kutumwa nchini Liberia kwa wanajeshi wa kulinda amani watakaofikia 15,000 kusaidia kuijenga upya nchi hiyo ya Afrika Magharibi baada ya takriban miaka 14 ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW