BEIJING:Mazungumzo ya Korea kaskazini yavunjika
22 Machi 2007Matangazo
Mazungumzo ya pande sita yenye nia ya kuishawishi Korea Kaskazini kuachana na mpango wake wa nuklia yamevunjika.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Bejing ambako ndiko kunakofanyika mazungumzo hayo, mwakilishi wa Korea Kaskazini, amerundi nyumbani.
Mazungumzo hayo yalianza hapo siku ya Jumatatu, yakiwa na nia ya kufanyia kazi makubaliano yaliyofikiwa mwezi uliyopita.Hata hivyo Korea Kaskazini imekuwa ikisisitiza irejeshewe fedha zake kiasi cha dola millioni 25 zilizozuiwa katika benki huko Macau.
Mapema wiki hii Marekani ilikubali kuwa kiasi hicho kinaweza kuachiwa, lakini haijafahamika wazi kwanini fedha hizo hazijarejeshwa Korea Kaskazini.