BEIJING:Tarehe maalum kwa Korea Kaskazini kufunga mitambo ya nuklia haijafikiwa
20 Julai 2007Matangazo
Siku ya tatu ya mazungumzo juu ya vinu vya nuklia vya Korea Kaskazini, yamemalizika bila ya kuwekwa tarehe maalum kwa nchi hiyo kufunga vinu vyake.
Ilitarajiwa ya kwamba mazungumzo hayo yangetoa mwongozo wa kitaalam juu ya hatua zaidi za kufunga vinu hivyo.
Katika mazungumzo ya pande sita mjini Beijing, mwakilishi wa Marekani kwenye mazungumzo hayo Christopher Hill alisema kuwa anaamini kuwa Korea Kaskazini itaweza kukamilisha awamu ya pili ya ufungaji wa vinu vyake itakapofika mwisho wa mwaka huu.