1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT : Hezbollah kutosalimisha silaha

23 Septemba 2006

Kiongozi wa kundi la Hezbollah Sheikh Hassan Nasrallah amejitokeza hadharani kwa mara ya kwanza tokea vita vya kundi hilo na Israel katika maandamano makubwa ya kushehereka ushindi hapo jana na kukataa wito wa kusalimisha silaha na kusema kwamba kundi la wapiganaji wake bado lina maroketi 20,000.

Nasrallah amejitokeza hadharani baada ya kuwa mafichoni kwa zaidi ya miezi miwili na kuhutubia mamia na maelfu ya wafuasi wake na wapiganaji waliokusanyika kwa maandamano hayo ya ushindi.Ametangaza kwamba Hezbollah imejipatia ushindi wa kihistoria na wa kivita dhidi ya Israel na kwamba hivi sasa lina nguvu kubwa kabisa kuwahi kuwa nazo.

Nasrallah ambaye anaonekana kuwa shujaa kwa Waarabu wengi na adui nambari moja kwa Israel amesema hawataki kuendelea kushikilia siliha milele lakini kundi lake halitosalimisha silaha zake kwa kadri taifa la Lebanon litakapoendelea kuwa dhaifu kwa kutokuwa na uwezo wa kujihami dhidi ya Israel.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW