1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT : Hizoballah kupambana kuendelea kushikilia silaha zake

26 Mei 2005

Ikiwa chini ya shinikizo la kimataifa linaloongezeka la kutaka wasalimishe silaha kundi la Hizbollah nchini Lebanon limesema hapo jana lina zaidi ya maroketi 12,000 ambayo yanaweza kushambulia po pote pale kaskazini mwa Israel na itapambana na yoyote yule anayejaribu kuwapokonya silaha.

Mkuu wa Hizbollah Sheikh Hassan Nasrullah amewaambia waandishi wa habari katika maadhimisho ya miaka mitano ya kujitowa kwa Israel kusini mwa Lebanon kwamba mkono wowote ule utakaozifikia silaha zao ni mkono wa Israel ambao utakatwa.

Amesema hawataki kumshambulia yoyote yule na hawatoruhusu yoyote kuishambulia Lebanon lakini iwapo mtu yoyote yule anafikiria kulipokonya silaha kundi hilo watapambana nao kama vile walivyofanya mashahidi wa Kerbala akimaanisha vita katika historia ya Kiislam ambao ndio msingi wa madhehebu ya Shia.

Amesema wazo lolote lile la kulipokonya silaha kundi hilo ni wendawazimu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW