BEIRUT : Israel yaendelea kushambulia Lebanon
12 Agosti 2006Matangazo
Licha ya kupitishwa kwa azimio la Umoja wa Mataifa hapo jana lenye kutaka kukomeshwa kwa mapigano nchini Lebanon jeshi la Israel limeanzisha operesheni ya mashambulizi makubwa kusini mwa Lebanon.
Mashambulizi hayo yameharibu mtambo wa umeme katika mji wa Sidon na watu 15 imeripotiwa kuwa wameuwawa au kujeruhiwa katika kijiji cha Rashaf kilomita 20 mashariki mwa mji wa Tyre.
Mapema shammbulio la anga la Israel lililolenga msafara wa magari ya raia waliokuwa wakiukimbia mji wa Marjayoun limeuwa takriban watu wanne na kujeruhi wengine 40.Raia hao walikuwa kwenye magari yanayofikia 1,000 yaliokuwa yakisafiri kuelekea kaskazini yakisindikizwa na wanajeshi wa Lebanon.
Israel imetowa taarifa ikisema kwamba hakiruhusu msafara huo.