1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT: Israel yaendelea kusihambuliaLebanon

19 Julai 2006

Vituo karibu na uwanja wa ndege wa Beirut na kusini mwa Lebanon,vimeshambuliwa na ndege za kivita za Israel,kwa siku ya nane kwa mfululizo.Israel ikiendelea na operesheni kuu ya kijeshi dhidi ya Hezbollah kusini mwa Lebanon, miripuko miwili iliutikisa mji mkuu Beirut mapema leo hii.Inadhaniwa kuwa miripuko hiyo imetokea kwenye vitongoji vilivyo kusini mwa Beirut,ambalo ni eneo la Hezbollah,lililoteketezwa vibaya sana tangu Israel kuanzisha operesheni yake ya kijeshi dhidi ya Lebanon wiki iliyopita.Ndege za Israel zimeshambulia daraja moja vile vile katika mji wa Sidon kusini mwa Lebanon.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW