BEIRUT : Israel yaonya wakaazi wasirudi kusini ya Lebanon
15 Agosti 2006Matangazo
Ndege za kivita za Israel zimedondosha vipeperushi juu ya anga ya kusini mwa Lebanon leo hii vikiwaonya wakaazi kutorudi nyumbani kabla ya kuwekwa kwa majeshi ya Israel na Lebanon kwenye eneo hilo.
Hii ni mara ya kwanza kwa vipeperushi vya Israel kudondoshwa katika eneo hilo la kusini tokea azimio la Umoja wa Mataifa kuamuru kusitishwa kwa mapigano. Vipeperushi hivyo vimewaonya wakaazi wasirudi katika maeneo ya kusini kabla ya kuwekwa kwa wanajeshi wanaotakiwa kulinda usalama wao.
Jeshi la Israel linapanga kuondoka kusini mwa Lebanon katika kipindi kisichozidi siku 10 na kukabidhi baadhi ya maeneo iliyoyateka kwa wanajeshi wa Umoja wa Mataifa katika masaa yasiozidi 48.