1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT: Juhudi za kuwahamisha watu kutoka Lebanon zaendelea

19 Julai 2006

Marekani na mataifa mengine yameanza kuwaondoa raia wao kutoka Lebanon hii leo, huku maelfu ya watu wakiyakimbia mashambulio ya angani ya jeshi la Israel kwa njia yoyote inayowezekana.

Umoja wa Mataifa umeonya juu ya mkasa mkubwa wa kibinadamu ambao tayari umewalazimu watu nusu milioni kupoteza makazi yao.

Wamarekani wamekusanyika karibu na ubalozi wao kazkazini mwa Beirut wakisubiri kuchukuliwa kwa basi kupelekwa bandari ya Beirut kupanda meli zitakazowahamisha nchini Lebanon. Meli tisa za jeshi la Marekani helikopta, na meli inayoweza kutumiwa na ndege kutua vitatumiwa kuwahamisha wamarekani zaidi ya 2,400.

Takriban Wabelgiji 200 wanasubiri kupanda mabasi mjini Beirut kukimbilia eneo la mpakani na Syria. Maelfu ya walebanon na raia wa kigeni wamo njiani kuelekea Syria kukimbia mashambulio ya mabomu ya jeshi la Israel.

Balozi wa Marekani kisiwani Cyprus, Oronald Schlicher, amesema wafanyikazi wa ubalozi wamepata vyumba katika hoteli na wamepata nafasi kwenye shule ambako kunajengwa kambi ya kuwahifadhi wamarekani wanaokimbia mapigano.

Waaustralia takriban 350 wanasubiri kupanda mabasi mjini Beirut na kupelekwa kwenye meli itakayowapeleka Uturuki.

Wakati huo huo, meli ya jeshi la Uingereza iliyokuwa imewabeba waingereza wanaokimbia Lebanon, imewasili kisiwani Cyprus leo. Waziri mkuu wa Uingereza bwana Tonya Blair amesema, ´Meli ya kwanza itafika leo kwa hiyo tutaweza kuwaondoa watu wengi. Sasa tuna meli sita katika eneo hilo. Tuna kikosi maalumu mjini Beirut. Tutafanya kila linalowezekana kuwaondoa raia wetu haraka iwezekanavyo.´

Raia wa Ujerumani wamerudishwa nyumbani na serikali imesema itawarudisha raia wengine kutoka Lebanon katika siku chache zijazo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW