BEIRUT: Kofi Annan ziarani Lebanon
28 Agosti 2006Matangazo
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Kofi Annan anakutana na waziri mkuu wa Lebanon,Fouad Siniora na spika wa Bunge Nabih Berri kujadiliana masharti ya azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu Lebanon.Miongoni mwa masharti hayo ni kupelekwa kwa kikosi cha kimataifa cha wanajeshi 15,000 nchini Lebanon.Kwa maoni ya wataalamu wa Umoja wa Mataifa,hadi mwishoni mwa juma,kiasi ya wanajeshi 3,500 watapelekwa Lebanon.Kikosi hicho kinatazamiwa kushirikiana na kikosi cha amani cha Umoja wa Mataifa cha wanajeshi 2,000 waliopo Lebanon.