1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT: Kundi la Hizbolah lajiunga na baraza la mawaziri nchini Lebanon

20 Julai 2005

Kundi la waislamu wa madhehebu ya shia nchini Lebanon, Hizbollah, limejiunga na barraza la mawaziri la nchi hiyo.waziri mkuu Fuad Siniora hatimaye ametangaza serikali mpya baada ya majuma kadhaa ya mivutano. Serikali hiyo imeidhinishwa na rais Emile Lahoud ambaye aliyakataa mapendelezo mengine matatu yaliyowasilishwa hapo awali.

Marekani imeapa haitafanya kazi na mwanachama wa Hizbolah katika baraza hilo la mawaziri. Msemaji wa wizara ya ndani ya Marekani amesema kwamba serikali ya Washington inalitambua kundi la Hizbola kuwa la kigaidi na sera yake juu ya kundi hilo bado haijabadilika.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW