1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT: Lahoud akosoa kuwapokonya silaha Hezbollah

17 Agosti 2006

Rais wa Lebanon, Emile Lahoud, ameukosoa mpango wa kuwapokonya silaha wanamgambo wa kundi la Hezbollah.

Kiongozi huyo, anayeegemea upande wa Syria, amesema ni aibu kulitaka kundi la Hezbollah liweke silaha zake chini hasa ikizingatiwa kwamba Hezbollah ni kikosi pekee katika mataifa ya kiarbu kinachoweza kupambana na Israel.

Marekani imesema kupokonywa silaha kundi la Hezbollah kutachukua muda na ni jukumu la serikali ya Lebanon kulifanikisha jambo hilo.

Wakati huo huo, Saad Hariri, mbunge wa Lebanon anayeipinga Syria, amemlaumu rais wa Syria, Bashar al Assad, kwa kuchochea vita nchini Lebanon.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW