1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT: Lebanon itatoa ombi rasmi kuhusu mchango wa Ujerumani

5 Septemba 2006

Waziri mkuu wa Lebanon,Fouad Siniora amesema,serikali yake inatayarisha mswada wa barua itakayopelekwa Umoja wa Mataifa ikiwa na ombi rasmi kuitaka Ujerumani ichangie wanajeshi wake katika kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Lebanon.Siniora ametoa tangazo hilo baada ya Ujerumani kuahirisha uamuzi wa kupeleka vikosi vya wanamaji kuungana na wanajeshi wa Umoja wa Mataifa.Ujerumani imekuwa ikingojea kupata ombi rasmi la kutuma vikosi vyake.Kwa upande mwingine,bunge la Uturuki leo hii litapiga kura juu ya uamuzi wa serikali kuchangia wanajeshi wake kama sehemu ya vikosi vya Umoja wa Mataifa kulinda amani nchini Lebanon.Raia wa Uturuki wamegawana katika maoni yao kuhusu suala hilo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW