BEIRUT: Majeshi ya Lebanon kulinda eneo la kusini
18 Agosti 2006Vikosi vya Lebanon vimepelekwa kusini mwa nchi kwa mara ya kwanza tangu miaka 38.Vikosi hivyo vitakuwepo kusini mwa mto wa Litani,eneo ambalo hadi hivi sasa lilidhibitiwa na wanamgambo wa Hezbollah.Wakati huo huo majeshi ya Kiisraeli yameondoka kutoka baadhi ya maeneo yaliyoikalia baada ya vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa kukabidhiwa sehemu hizo.Licha ya shinikizo la kimataifa,serikali ya Lebanon imepuza suala la kuwanyanganya silaha wanamgambo wa Hezbollah.Hilo ni sharti mojawapo muhimu la kusitishwa mapigano kati ya Israel na Hezbollah.Kwa upande mwingine ndege za mwanzo za abiria zimetua kwenye uwanja wa ndege wa Beirut. Uwanja huo pia ulishambuliwa na Israel na ulifungwa wakati wa vita.Katika mgogoro huo wa majuma manne si chini ya watu 1,100 wameuawa nchini Lebanon na Waisraeli 157 pia waliuliwa.