BEIRUT: Marekani yapeleka misaada Lebanon
26 Mei 2007Matangazo
Ndege kadha za kijeshi za Marekani zimetua katika Uwanja wa Ndege wa Beirut zikiwa na misaada ya kijeshi kutoka Marekani na mataifa washirika ya Kiarabu.
Misaada hiyo imepelekewa majeshi ya Lebanon kutokana na wito uliokuwa umetolewa na serikali hiyo.
Serikali ya Lebanon pia imepeleka vikosi vya ziada kwenye kambi ya wakimbizi wa Kipaletina ya Nahr al-Bared kaskazini mwa nchi hiyo ambako majeshi yamekuwa yakipambana na wanamgambo wa Kiislamu.