1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT: Mmuagiko wa damu waendelea kusini mwa Lebanon

25 Julai 2006

Familia ya Ki-Lebanon ya watu 7 imeuawa na kombora la Israel kusini mwa Lebanon,huku vikosi vya Kiisraeli vikiendelea na mashambulio yake ya mabomu dhidi ya wanamgambo wa Hezbollah.Israel pia imesema kuwa imeuteka mji wa Bint Jbeil,ambao ni ngome ya wanamgambo wa Hezbollah,kusini mwa Lebanon.Kwa mujibu wa msemaji wa majeshi ya Kiisraeli,vikosi na vifaru vimeuzingira mji huo.Amesema,lengo ni kuzuia makombora yanayorushwa na Hezbollah katika miji ya Kiisraeli.Wa-Lebanon waliokimbilia Cyprus wanasema wana khofu kuwa familia na marafiki walioachwa nyuma wanapungukiwa na vyakula.Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa kutaanzishwa operesheni ya kupeleka misaada.Mratibu mkuu wa misaada ya kiutu wa Umoja wa Mataifa,Jan Egeland amesema leo hii anakwenda Israel kuihimiza serikali ya nchi hiyo iruhusu misafara ya magari kupeleka misaada kwa usalama.Tangu mgogoro huo kuanza majuma mawili yaliyopita,si chini ya Wa-Israeli 41 na Wa-Lebanon 390 wameuawa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW