BEIRUT: Prodi aahidi kuiunga mkono Lebanon
11 Oktoba 2006Matangazo
Waziri mkuu wa Italia, Romano Prodi amekutana na waziri mkuu wa Lebanon, Fuad Siniora mjini Beirut hii leo. Viongozi hao wamezungumzia jeshi la kimataifa la kulinda amani kusini mwa Lebanon litakaloongozwa na Italia.
Prodi ameahidi kusaidia kuidumisha Lebanon, pamoja na juhudi za kubadilishana wafungwa na Israel. Aidha Prodi amesema Itali itasaidia juhudi za kisiasa na ujenzi.
Akizungumza kuhusu mabadilishano ya wafungwa kati ya Lebanon na Israel, Romano Prodi amesema amelijadili swala hilo na spika wa bunge la Lebanon, Nabih Berri, aliyepewa jukumu na kundi la Hezbollah ayashughulikie mazungumzo juu wafungwa. Prodi amesema kulitanzua tatizo hilo kutasaidia kurejesha amani.