1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT: Shambulio la Israel limeua wanajeshi wa Umoja wa Mataifa

26 Julai 2006

Wanajeshi 4 wa Umoja wa Mataifa wameuawa katika shambulio la angani lililofanywa na Israel.Duru za Umoja wa Mataifa,zimesema kuwa kituo cha uangalizi katika mji wa Khiam,kusini mwa Lebanon kilishambuliwa.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan amesema ameshtushwa na kile alichokiita kuwa ni ”kitendo cha kuwalenga makusudi wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa”.Israel imesema inasikitishwa na tukio hilo na itafanya uchunguzi.Kwa upande mwingine,jeshi la Israel limesema kuwa vikosi vyake vimemuua kamanda wa Hezbollah wa ngazi ya juu,Abu Jaafar na vimeuteka mji wa Bint Jubeil unaodhaniwa kuwa ni ngome ya wanamgambo wa Hezbollah.Wakati huo huo,wapiganaji wa Hezbollah wamevurumisha makombora dazeni kadhaa katika miji iliyo kaskazini mwa Israel.Mashambulio hayo yamemuuwa mtu mmoja na kujeruhi zaidi ya 20.Kiongozi wa Hezbollah,Hassan Nasrallah katika hotuba iliyotangazwa kwenye televisheni,ameionya Israel kuwa wanamgambo wake sasa wapo tayari kushambulia vituo vilivyo kusini mwa mji wa Haifa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW