1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT : Ufaransa kuchangia wanajeshi 2,000

25 Agosti 2006

Ufaransa imesema iko tayari kuchangia jumla ya wanajeshi 2,000 kwa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa kusimamia usitishaji wa mapigano nchini Lebanon.

Rais Jaques Chirac amesema hakikisho la Umoja wa Mataiafa kwamba wanajeshi wa Ufaransa watakuwa wanaweza kujihami wao wenyewe na kuwalinda raia limewafanya wabadili uamuzi wao wa awali.

Awali Ufaransa ilivunja matarajio ya Umoja wa Mataifa kwa kuwa tayari kutowa wanajeshoi 400 tu kwa shughuli hizo na kukifanya kikosi hicho cha kimataifa kukabiliwa na upungufu mkubwa wa wanajeshi 15,000 wanaotakiwa kuunda kikosi hicho.

Italia ambayo imeahidi kutowa wanajeshi 3,000 na kuwa tayari kuongoza shughuli za kulinda amani Lebanon imesema imeridhiwa na Marekani.